Ethiopia yarejesha tena huduma za internet baada ya kuwepo kwa utulivu
Serikali ya Ethiopia alhamisi ilirejesha tena huduma za internet baada ya kusitisha tangu Juni 29 kufuatia ghasia zilizozuka katika mji mkuu Addis Ababa na sehemu nyingine za nchi na kusababisha vifo vya watu takriban 239.
Maandamano makubwa yalizuka mjini Addis Ababa pamoja na miji mingine kadhaa ya Jimbo la Oromia wakati waandamaji wakionyesha hasira zao kutokana na kifo cha mwanamuziki maarufu wa Oromia Hachalu Hundessa, ambaye ameuawa Juni 29 na watu wasiojulikana.
Tukio hilo limepelekea kuzimwa kwa interenet, hatua ambayo serikali ya Ethiopia inasema imesaidia kudhibiti hali na kukabiliana na uharibifu usiotakiwa unaofanywa na waandamanaji ambao wana ajenda zao za siri.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |