Marais wa Tanzania na Uganda wakubaliana kuharakisha ujenzi wa bomba la mafuta
Rais John Magufuli wa Tanzania na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni wamesaini makubaliano yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 3.5 ya kujenga boma la mafuta lenye urefu wa kilometa 1,445 kutoka kwenye visima vya mafuta vya Hoima, Uganda hadi kwenye bandari ya Tanga, Tanzania.
Marais hao walisaini makubaliano hayo jana mjini Chato, na wamewataka maofisa wao kukamilisha haraka mambo yaliyobaki ili mradi huo uanze kutekelezwa. Rais Magufuli amesema imechukua muda mrefu kabla ya kukamilisha makubaliano hayo kutokana na unyeti wa mradi huo, na baada ya majadiliano ya miaka mingi sasa wamefikia makubaliano.
Mradi huo utakapokamilika unatarajiwa kuiwezesha Tanzania kupata dola za kimarekani bilioni 3.2 na kuzalisha kati ya ajira elfu 10 na elfu 15 katika kipindi cha miaka 25 ijayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |