Wafungwa 219 wametoroka kutoka gereza la Singila lililoko katika wilaya ya Moroto, kaskazini mashariki mwa Uganda.
Msemaji wa jeshi la magereza nchini humo Frank Baine amesema, wafungwa saba wamekamatwa tena na watatu wameuawa. Amesema vikosi vya jeshi la magereza, jeshi la ulinzi na polisi vinashirikiana kwa pamoja kuwakamata wafungwa waliotoroka.
Ameongeza kuwa wafungwa hao, wengi wakiwa wamehukumiwa kutokana na kumiliki isivyo halali silaha za moto, wamechukua bunduki 14 na risasi kadhaa wakati wanapotoroka.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |