• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 12-Septemba 18)

    (GMT+08:00) 2020-09-18 16:48:13
    Balozi wa China aeleza msimamo wa China kuhusu suala la Sudan Kusini

    Naibu Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing jumatano alieleza msimamo wa China kwenye mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu suala la Sudan Kusini uliofanyika kwa njia ya video, akisema China inafuatilia maendeleo ya hali ya Sudan Kusini.

    Kutokana na athari za janga la COVID-19 na kupungua kwa bei ya mafuta, hali ya kiuchumi na kibinadamu nchini humo imekuwa mbaya, na utekelezaji wa makubaliano ya kutatua mgogoro wa Sudan kusini inakabiliwa na changamoto nyingi.

    China imeipongeza Sudan Kusini kwa maendeleo iliyoyapata katika suala la upangaji wa majimbo, na kuzihimiza pande mbalimbali ziendelee na mazumgumzo kuhusu utekelezaji wa makubaliano hayo. China imezihimiza pande mbalimbali kushiriki kwenye pendekezo la kusimamisha vita lililotolewa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ili kulinda mazingira ya amani na utulivu kwa pamoja..

    Habari nyingine zinasema naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya kibinadamu Bw. Mark Lowcock ameonya kuhusu kuongezeka kwa tatizo la upungufu wa chakula nchini Sudan Kusini. Mwaka huu jumla ya watu milioni 7.5 nchini humo wanahitaji msaada wa kibinadamu.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  11  12  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako