Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) inasema hadi sasa Ethiopia ina wakimbizi wa ndani (IDPs) zaidi ya milioni 1.8.
Ripoti hiyo ina takwimu zilizokusanywa kati ya mwezi Juni na Julai kwenye maeneo 1,200 yanayohifadhi wakimbizi wa ndani na kwenye vijiji zaidi ya 1,200 vinavyotajwa kuwa watu hao wamerudi. Chanzo kikuu cha watu hao kuwa wakimbizi wa ndani ni migogoro iliyochangia asilimia 68 ya watu hao kukimbia makazi yao, na vyanzo vingine ni ukame na mafuriko.
IOM imesema itaendelea kufanya ufuatiliaji wa uhamiaji wa wakimbizi hao ili iweze kutoa takwimu zenye usahihi kwa serikali kuu, serikali za majimbo na serikali za mitaa ili kuwafuatilia watu hao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |