Msemaji wa serikali ya Tanzania Dr. Hassan Abbas hivi karibuni amesema, Tanzania inapongeza pendekezo la usalama wa data duniani lililotolewa na China ambalo linasaidia kuhimiza usimamizi na ushirikiano katika sekta hiyo.
Dr. Abbas amesema, pendekezo hilo linasaidia kulinda mamlaka ya nchi, na kupambana na kitendo cha kupata kiharamu data za watumiaji wa internet. Amesema, pendekezo hilo linaendana na kanuni ya kimsingi ya sheria ya kimataifa, na jamii ya kimataifa inapaswa kushikilia utaratibu wa pande nyingi katika sekta ya usimamizi wa data. Pia amesema, Tanzania inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa, kulinda kwa pamoja usalama wa data, kuhimiza maendeleo ya uchumi wa kidijitali, ili kuwanufaisha watu wengi zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |