• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Vita dhidi ya virusi vya Corona yaingia mashakani baada ya WHO kuingizwa kwenye masuala ya kisiasa 2020-04-15

    Rais Donald Trump wa Marekani, jana ametangaza kuwa nchi hiyo itasimamisha ufadhili kwa Shirika la Afya Duniani, (WHO). Rais Trump amelilaumu Shirika hilo kwa kutotoa habari kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona kwa wakati, kutotoa mapendekezo kuhusu kinga na udhibiti wa maambukizi, na kutotangaza hali ya maambukizi makubwa ya duniani. Rais Trump amesema, baada ya muda mrefu, ni wakati wa WHO kuwajibika. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa Chuo Kikuu cha John Hopkins, mpaka kufikia leo, idadi ya kesi za maambukizi ya virusi vya Corona duniani imefikia 1,986,986, na watu 126,812 wamefariki kutokana na virusi hivyo

    • UN: Ukuaji wa uchumi wa dunia kupungua kwa asilimia moja mwaka huu kutokana na virusi vya Corona 2020-04-02
    Ripoti iliyotolewa jana na Idara ya masuala ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa DESA imeonyesha kuwa, ukuaji wa uchumi wa dunia unaweza kupungua kwa asilimia moja mwaka huu kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona unaokithiri kote duniani, hali ambayo itakuwa mbaya zaidi kama hatua za kifedha zenye ufanisi hazitachukuliwa.
    • Maambukizi ya COVID-19 kote duniani kufikia milioni 1 ndani ya siku kadhaa 2020-04-02

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani Bw. Tedros Ghebreyesus amesema kuenea kwa kasi kwa virusi vya Corona kumesababisha ongezeko kubwa la maambukizi katika wiki kadhaa iliyopita, na idadi hiyo itafikia milioni 1 ndani ya siku kadhaa na idadi ya vifo itazidi elfu 50.

    • Idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona nchini Italia yazidi laki 1 2020-03-31

    Kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa na idara ya ulinzi wa raia ya Italia inayoshughulikia kazi ya kukabiliana na dharura ya taifa, hadi jana watu 11,591 wamefariki dunia nchini humo kutokana na virusi vya Corona, huku idadi ya watu walioambukizwa ikiongezeka hadi kufikia 101,739.

    • Mtaalam wa Marekani asema virusi vya Vorona vimetoka kwa asili
     2020-03-30

    Mtaalam wa virusi kutoka Chuo Kikuu cha Tulane nchini Marekani Profesa Robert Garry hivi karibuni alipohojiwa na Shirika la habari la nchi hiyo ABC alisema, kwa mujibu wa uchambuzi wao, soko la vyakula vya bahari mjini Wuhan, China sio chimbuko la virusi vya Corona, kauli ambayo imefuatiliwa sana na jamii ta kimataifa.

    • China na Marekani zapaswa kushirikiana katika mapambano dhidi ya COVID-19 2020-03-24

    Baada ya virusi vya Corona kuendelea kuenea, watu zaidi laki 3 wameambukizwa kote duniani. Lakini wakati nchi mbalimbali duniani zinashirikiana kupambana na virusi hiyo, serikali ya Marekani inatumia nguvu yake katika kulaumu China.

    • WHO yasema China kutokuwa na mgonjwa mpya wa COVID-19 ni mafanikio mkubwa 2020-03-20
    Katibu mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus jana huko Geneva amesema, China kutokuwa na mgonjwa mpya wa COVID-19 kwa mara ya kwanza ni mafanikio makubwa.
    • WHO yatoa wito kwa nchi za Ulaya kujifunza uzoefu wa China katika kupambana na COVID-19 2020-03-18

    Mkuu wa Shirika la afya duniani (WHO) barani Ulaya Bw. Hans Kluge ametoa wito kwa nchi za Ulaya kuchukua hatua za kijasiri zaidi za kuzuia nimonia ya COVID-19, na kusisitiza haja ya kuwahamasisha na kuwashirikisha watu wote katika kuzuia na kudhibiti janga hilo.

    • WHO yasema idadi ya wagonjwa wa COVID-19 duniani inakaribia laki 1.7 2020-03-17

    Shirika la afya duniani WHO limetoa ripoti ya kawaida ikisema, hadi kufikia jana asubuhi, nchi na kanda 152 zimeripoti watu 167,511 waliothibitishwa kuambukizwa COVID-19, idadi ambayo imeongezeka kwa watu 13,903 ikilinganishwa na siku iliyotangulia.

    • COVID-19 yasababisha upungufu wa uwekezaji wa moja kwa moja duniani 2020-03-09

    Ripoti iliyotolewa katika mkutano wa biashara na maendeleo wa Umoja wa Mataifa UNCTAD imeonyesha kuwa, kutokana na maambukizi ya COVID-19, uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje duniani katika mwaka 2020 unatarajiwa kupunguza kwa asilimia 5 hadi asilimia 15. Hata hivyo, ingawa China pia itaathiriwa na mazingira ya jumla ya uwekezaji duniani, maambukizi hayo hayatabadili hali ya kimsingi ya China kuvutia uwekezaji kutoka nje.

    • Uturiki yaeleza sababu za kufungua mpaka wake na kuwaruhusu wahamiaji kuingia Ulaya 2020-03-04

    Uamuzi wa Uturuki uliotolewa wiki iliyopita na rais Tayyip Erdogan wa kufungua mpaka wa nchi yake kuwaruhusu wahamiaji kukusanyika katika mpaka wa Ugiriki umepokelewa vibaya na baadhi ya wanasiasa wa Umoja wa Ulaya. Balozi wa Umoja wa Ulaya ameeleza kukasirishwa na hatua hiyo, na kusema uamuzi huo una lengo la kusaliti Umoja huo.

    • Mtaalamu wa China apendekeza kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya janga la nzige 2020-03-02

    Hivi karibuni jamii ya kimataifa imefuatilia kwa karibu janga la nzige katika Afrika, Asia ya Magharibi na Asia ya Kusini. Mtaalamu wa China Bw. Zhang Zehua anaona kuwa inapaswa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya janga hilo.

    • Makamu wa rais wa Iran athibitishwa kuambukizwa virusi vya korona 2020-02-28

    Makamu wa rais wa Iran anayeshughulikia mambo ya wanawake na familia Bibi Masoumeh Ebtekar jana amethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona.

    • Misri yamzika Mubarak kwa heshima za kijeshi 2020-02-27

    Misri imefanya mazishi ya heshima za kijeshi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak aliyefariki Jumanne akiwa na umri wa miaka 91. Mwili wa rais huyo wa zamani ulisafirishwa kwa ndege kwenye msikiti ulioko mashariki mwa New Cairo, ambako mazishi yake yalifanyika.

    • Idadi ya watu walioambukizwa COVID-19 nchini Italia yaongezeka na kufikia 322 2020-02-26

    Kamishna maalumu wa matukio ya dharura na mkuu wa idara ya ulinzi wa umma ya Italia Bw. Angelo Borrelli, ametangaza kuwa watu 322 wamethibitishwa kuambukizwa COVID-19 nchini humo, na 10 kati yao wamefariki dunia.

    • Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak afariki dunia 2020-02-26
    Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak amefariki dunia jana Jumanne, akiwa na umri wa miaka 91
    • Idadi ya watu walioambukizwa COVID-19 nchini Italia yaongezeka na kufikia 322 2020-02-26

    Kamishna maalumu wa matukio ya dharura na mkuu wa idara ya ulinzi wa umma ya Italia Bw. Angelo Borrelli, ametangaza kuwa watu 322 wamethibitishwa kuambukizwa COVID-19 nchini humo, na 10 kati yao wamefariki dunia.

    • Idadi ya vifo kutokana na virusi vya korona nchini Italia yafikia saba 2020-02-25

    Idadi ya vifo kutokana na virusi vya korona nchini Italia imeongezeka na kufikia 7 baada ya mkoa wa kaskazini wa Lombardy kutangaza kifo cha mwanaume mwenye umri wa miaka 62 jana usiku.

    • Waziri mkuu wa Malaysia ajiuzulu
     2020-02-24

    Ofisi ya waziri mkuu wa Malaysia imetangaza kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Mahathir Mohamad amewasilisha barua ya kujiuzulu wadhifa huo kwa kiongozi wa nchi hiyo.

    • Shirika la ndege la Iraq lasimamisha safari za ndege kwenda Iran kutokana na COVID-19 2020-02-21
    Shirika la ndege la Iraq limesimamisha safari za ndege kwenda na kurudi kutoka Iran ikiwa ni hatua ya kuzuia maambukizi ya virusi vya COVID-19 baada ya kutokea nchini Iran. Uamuzi huo umetolewa na wizara ya uchukuzi baada ya wizara ya afya ya Iran kutoa mapendekezo ya kuchukua hatua za lazima za kuzuia maambukizi ya virusi hivyo nchini Iraq.
    prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako