• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Kundi la IS latangaza kuwajibika na shambulizi dhidi ya tume ya uchaguzi Libya 2018-05-03

    Kundi la Islamic State limekiri kufanya shambulizi la kujitoa mhanga dhidi ya makao makuu ya tume ya uchaguzi ya Libya mjini Tripoli. Kundi hilo pia limesema shambulizi hilo linatokana na amri ya msemaji wa kundi hilo Abu Hassan al-Muhajir, na limesababisha vifo vya wanausalama na wafanyakazi zaidi ya 15 wa tume hiyo.

    • Mtu mmoja auawa na mwingine kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la risasi jijini London 2018-05-02

    Vyombo vya habari mjini London, Uingereza, vimesema mtu mmoja ameuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la risasi lililotokea jana usiku kaskazini magharibi mwa mji wa London.

    • Rais wa korea Kusini autaka Umoja wa Mataifa kufuatilia mpango wa Korea Kaskazini wa kufunga vituo vya majaribio ya nyuklia
     2018-05-01

    Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini ameutaka Umoja wa Mataifa kufuatilia mpango wa Korea Kaskazini wa kufunga vituo vyake vya majaribio ya nyuklia.

    • Idadi ya watu waliouawa katika mashambulizi mawili ya mabomu nchini Afghanistan yafikia 23
     2018-04-30

    Watu 23 wameuawa wakiwemo washambuliaji wawili na wengine 27 kujeruhiwa katika mashambulizi mawili ya mabomu yaliyotokea kwenye eneo lenye ofisi za balozi za nchi za nje katikati ya mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, leo asubuhi.

    • Pendekezo la Ukanda moja na Njia moja linasaidia ongezeko la uchumi la nchi husika 2018-04-19

    Zaidi ya asilimia 90 ya benki kuu za nchi 26 zilizoko kwenye Ukanda Mmoja na Njia Moja zinaona kuwa pendekezo hilo litasaidia kuhimiza uchumi wao katika miaka 5 ijayo, na nchi nyingi ziliunga mkono mashirika ya pande mbalimbali yaliyoongozwa na China.

    • Saudi Arabia yashauriana na Marekani kuhusu kutuma jeshi nchini Syria 2018-04-18

    Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Adel al-Jubeir amesema, nchi hiyo inashauriana na Marekani kuhusu kutuma jeshi nchini Syria.

    • Mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria wazuia makombora mengi yaliyolenga viwanja viwili vya jeshi la anga 2018-04-17
    Vyombo vya habari vya Syria vimeripoti kuwa, mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria umefanikiwa kuzuia makombora mengi yaliyolenga viwanja viwili vya jeshi la anga nchini Syria leo alfajiri.
    • Mazungumzo ya 4 ya ngazi ya juu ya uchumi kati ya China na Japan yafanyika 2018-04-16

    Mjumbe wa taifa ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na mwenzake wa Japan Bw. Kouno Tarou leo huko Tokyo wameendesha mazungumzo ya nne ya ngazi ya juu ya uchumi kati ya China na Japan.

    • Marekani yaanza kushambulia maeneo ya Syria, milipuko yasikika 2018-04-14
    Marekani imeanza mashambulizi dhidi ya Syria katika mji mkuu wa Damascus kabla siku ya jumamosi ambapo milio mikali yenye miale miekundu ya mabomu ilionekana katika anga.

    Milio ya sauti za milipuko ilisikika katika mji mkuu huo katika maeneo yote, huku majeshi ya anga yaSyria nayo yakionekana kurusha makombora yake kutokea mlima Qasion, ambao unatazamamana na mji mkuu wa Damascus.

    • Marekani hakika itashindwa kwenye vita ya kibiashara inayotaka kufanya na China kutokana na makosa yake matatu 2018-04-08

    Historia huwa haijirudii, lakini huweza kueleza. Wakati serikali ya Trump inapotishia China kwa fimbo la mgogoro wa kibiashara, watu wanaweza kukumbuka kauli maarufu aliyoitoa Jenerali Omar Bradley tarehe 15, Mei mwaka 1951 bungeni akiwa mwenyekiti wa wanadhimu wakuu kwa wazo la kutaka kupanua Vita ya Korea hadi China. Kauli hiyo ni kuwa "itakuwa ni vita isiyofaa, katika sehemu isiyofaa, katika wakati usiofaa na dhidi ya adui asiyefaa" Hivi sasa, serikali ya Trump inataka kuanzisha vita ya biashara na China, jambo ambalo pia amefanya makosa matatu na hakika Marekani itashindwa katika vita hiyo.

    • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aunga mkono utandawazi duniani na mfumo wa biashara wa pande mbalimbali 2018-04-06

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana alifafanua kuwa vitendo vya kujilinda kibiashara si njia sahihi ya kutatua mivutano ya biashara, na pia alieleza kuunga mkono utandawazi duniani na mfumo wa biashara wa pande mbalimbali.

    • Mkutano wa usalama wa kimataifa wafuatilia mfumo wa usalama wa kimataifa na mapambano dhidi ya ugaidi 2018-04-05

    Mkutano wa 7 wa usalama wa kimataifa umefanyika jana mjini Moscow, Russia, ambapo wajumbe waliohudhuria mkutano huo walijadili mwelekeo wa kufanya juhudi katika kupambana na ugaidi katika siku zijazo na kusisitiza kulinda mfumo wa usalama wa kimataifa na maelewano, haki na usawa.

    • China yatarajia jumuiya ya kimataifa kuendelea kutoa mchango kuboresha hali ya Haiti 2018-04-04

    Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema, jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuendelea kutoa mchango kuboresha hali ya Haiti na kuhimiza pande zote za nchi hiyo kuongeza nguvu kuendeleza uchumi wao na kuboresha maisha ya watu.

    • Raia elfu 40 warejea Ghouta Mashariki nchini Syria
     2018-04-03

    Jumla ya raia elfu 40 wamerejea kwenye makazi yao katika eneo la Ghouta Mashariki, pembezoni mwa mji mkuu wa Syria, Damascus, ambapo jeshi la serikali linakaribia kuukomboa mji huo.

    • Russia yafanikiwa kufanya jaribio la mfumo mpya wa kisasa wa kupambana na makombora 2018-04-02

    Jeshi la Russia limefanikiwa kufanya jaribio la mfumo mpya wa kisasa wa kupambana na makombora nchini Kazakhastan.

    • China yatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia Afrika kuongeza uwezo wake wa kulinda amani na usalama 2018-03-23

    Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Ma Chaoxu ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuisaidia Afrika kuongeza uwezo wake wa kulinda amani na usalama.

    • Korea Kusini kupendekeza kufanya mkutano wa ngazi ya juu kati yake na Korea Kaskazini wiki ijayo 2018-03-22
    Korea Kusini imeamua kupendekeza kufanya mkutano wa ngazi ya juu na Korea Kaskazini tarehe 29 mwezi huu, na kufanya maandalizi ya mkutano wa viongozi utakaofanyika mwezi ujao.
    • Mkutano wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu wa G20 wafunguliwa 2018-03-20

    Mkutano wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu wa kundi la G20 umeanza jana huko Buenos Aires nchini Argentina.

    • Putin achaguliwa tena kuwa rais wa Russia 2018-03-19

    Tume Kuu ya Uchaguzi ya Russia imesema, rais wa sasa wa Russia Vladmir Putin amepata asilimia 76.6 za kura baada ya asilimia 99.83 ya kura kuhesabiwa katika uchaguzi wa rais uliofanyika jana.

    • Rais wa Marekani anapanga kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini 2018-03-09

    Rais Donald Trump wa Marekani amesema anapanga kukutana na kiongozi wa juu wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong-un.

    prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako