• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya ndege ya abiria nchini Kazakhstan yafikia 15 2019-12-27

    Mamlaka ya usafiri wa anga nchini Kazakhastan imesema, idadi ya watu waliofariki katika ajali ya kuanguka kwa ndege imefikia 15.

    • Marekani yafikiria kuondoa askari wake kutoka nchi za Afrika magharibi 2019-12-25

    Gazeti la New York Tims jana liliripoti kuwa, waziri wa ulinzi wa taifa wa Marekani Bw. Mark Esper anafikiria mpango wa kuondoa askari wa nchi hiyo kutoka nchi za Afrika magharibi, ambao ni sehemu moja ya mpango wa kupunguza tena askari 200,000 waliopo nchi za nje.

    • Boris Johnson aapishwa rasmi kuwa waziri mkuu wa Uingereza 2019-12-14

    Kiongozi wa Chama cha Kihafidhina cha Uingereza Bw. Boris Johnson jana aliapishwa rasmi kuwa waziri mkuu wa Uingereza baada ya kushinda kwenye uchaguzi wa Baraza la chini la bunge la Uingereza.

    • Umoja wa Afrika watoa mwito wa kukabiliana na mzigo unaosababishwa na ugonjwa wa UKIMWI kwa makundi dhaifu 2019-12-02
    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat ametoa wito wa kuwepo kwa juhudi za makusudi kupunguza mzigo wa ugonjwa wa UKIMWI kwa watu wazima walioko kwenye makundi yaliyo hatarini, hasa wakimbizi, watu wanaorudi makwao na wakimbizi wa ndani.
    • Korea Kaskazini yarusha makombora mawili yasiyotambulika kwenye Bahari ya Mashariki
     2019-11-28

    Wanadhimu Wakuu wa Majeshi ya Korea Kusini wamesema, Korea Kaskazini imerusha makombora mawili yasiyotambulika katika Bahari ya Mashariki.

    • Rais wa China atetea utaratibu wa pande nyingi kwenye mkutano wa BRICS
     2019-11-15

    Mkutano wa 11 wa viongozi wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini zinazounda kundi la BRICS umefanyika mjini Brasilia, Brazil, na kuhudhuriwa na marais Jair Bolsonaro wa Brazil, Xi Jinping wa China, Vladmir Putin wa Russia, Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na waziri mkuu wa India Narendra Modi. Rais Xi amehutubia ufunguzi wa mkutano huo akizihimiza nchi hizo kubeba majukumu ya kutetea na kutekeleza utaratibu wa pande nyingi.

    • Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG lasaini makubaliano na Shirika la Utangazaji la Brazil EBC 2019-11-15
    Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG na Shirika la Utangazaji la Brazil EBC EBC zimesaini makubaliano ya ushirikiano. Kutokana na makubaliano hayo, pande mbili zitafanya ushirikiano wa pande zote katika kubadilishana maudhui, kutengeneza na kusambaza vipindi kwa pamoja, maingiliano ya watu, na teknolojia za radio, televisheni na vyombo vipya vya habari vya 5G.
    • Wahanga wote wa tukio la Essex wamethibitishwa kuwa ni raia wa Vietnam 2019-11-08

    Wizara ya usalama wa umma ya Vietnam imethibitisha kuwa wahanga wote 39 waliokutwa wamekufa ndani ya lori katika kaunti ya Essex nchini Uingereza wamethibitishwa kuwa ni raia wa Vietnam. Wizara hiyo imesema watu hao wanatoka katika maeneo sita ya Vietnam.

    • Serikali ya Yemen na STC zasaini makubaliano ya kugawana madaraka 2019-11-06

    Serikali ya Yemen na kamati ya mpito ya kusini STC zimesaini makubaliano ya kugawana madaraka huko Riyadh, Saudi Arabia.

    • Nchi 54 zaunga mkono hatua za China za kukabiliana na ugaidi mkoani Xinjiang 2019-10-30
    Nchi 54 zimetangaza kwa pamoja kuunga mkono hatua za China cha kukabiliana na ugaidi na msimamo mkali katika Mkoa Unaojiendesha wa Xinjiang Uygur.
    • Bibi Tu Youyou atunukiwa tuzo na UNESCO 2019-10-23
    Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limetangaza orodha ya washindi wa tuzo ya kimataifa ya utafiti wa sayansi ya maisha, kwa ajili ya mashirika au watu waliotoa mchango muhimu katika kuboresha ubora wa maisha ya watu. Orodha ya mwaka huu ina watu watatu akiwemo Tu Youyou wa China aliyegundua dawa ya Artemisinin, na kuokoa maisha ya mamilioni ya watu.
    • Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya wapitisha makubaliano mapya kuhusu Uingereza kujitoa umoja huo 2019-10-18
    Viongozi wa nchi 27 za Umoja wa Ulaya isipokuwa Uingereza jana wamefikia makubaliano na kupitisha azimio la kuunga mkono makubaliano mapya yaliyofikiwa kati ya kamati ya umoja huo na serikali ya Uingereza.
    • IMF yapunguza makadirio ya ongezeko la uchumi kwa mwaka huu 2019-10-16

    Shirika la fedha duniani IMF limetoa Ripoti ya Makadirio kuhusu Uchumi wa Dunia, likipunguza makadirio ya ongezeko la uchumi wa dunia kwa mwaka 2019 hadi asilimia 3, ambayo imepunguzwa kwa asilimia 0.2 ikilinganishwa na makadirio yaliyotolewa mwezi Julai. Hiki pia ni kiwango cha chini zaidi tangu msukosuko wa fedha ulipuke mwaka 2008.

    • Mazungumzo ya ngazi ya juu ya biashara kati ya China na Marekani yamalizika mjini Washington 2019-10-12

    Naibu waziri mkuu wa China ambaye pia ni kiongozi wa China kwenye mazungumzo ya kiuchumi kati ya China na Marekani Liu He, mjumbe wa biashara wa Marekani Robert Lighthizer, na waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin walifanya mazungumzo ya raundi mpya kuhusu uchumi na biashara kuanzia tarehe 10 hadi 11 mwezi huu huko Washington.

    • Waziri mkuu wa Japan atarajia ziara itakayofanywa na rais wa China nchini humo kufungua ukurasa mpya kati yao 2019-10-03

    Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ametoa pongezi kwa miaka 70 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China na kutarajia uhusiano kati ya nchi hizo mbili uwe na mustakabali mzuri zaidi.

    • Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac afariki dunia 2019-09-27
    Rais wa zamani wa Ufaransa Bw. Jacques Chirac amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86. Mwanasiasa huyo wa mrengo wa kulia na kati alikuwa anajulikana zaidi kwa kuamua kupinga operesheni ya kijeshi dhidi ya Iraq ya mwaka 2003 iliyoongozwa na Merekani. Uamuzi huo ulimletea heshima nchini mwake, lakini ulidhuru uhusiano wa kidiplomasia kati ya Ufaransa na Marekani.
    • Georgieva wa Bulgaria ateuliwa mkurugenzi wa IMF 2019-09-26
    Bodi ya utendaji ya Shirika la Fedha la Kimataifa IMF imeidhinisha uteuzi wa Kristalina Georgieva raia wa Bulgaria aliyekuwa ofisa mtendaji wa Benki ya Dunia, kuwa mkurugenzi wa shirika hilo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Oktoba Mosi.
    • Juncker asema Umoja wa Ulaya hauwajibiki na matokeo ya Brexit 2019-09-23

    Mwenyekiti wa Kamati ya Ulaya Bw. Jean Claude Juncker amesema Umoja wa Ulaya hauwajibiki na matokeo ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja huo, na kwamba Umoja huo haupaswi kulaumiwa kwa uamuzi wa Uingereza.

    • Kiongozi wa Iran asisitiza nchi yake haitafanya mazungumzo na Marekani 2019-09-18

    Kiongozi wa Iran Ali Khamenei jana alisisitiza kuwa, Iran haitafanya mazungumzo ya ngazi yoyote na Marekani. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika la habari la kiserikali la nchi hiyo, Khamenei amesisitiza kuwa Marekani imekuwa na matumaini ya kufanya mazungumzo na Iran ili kuilazimisha Iran ipokee nia yake

    • Uturuki, Russia na Iran zafuatilia hali ya Idlib nchini Syria 2019-09-17

    Uturuki, Russia na Iran zinafuatilia suala la usalama nchini Syria wakati wa mazungumzo kati ya pande hizo tatu, na kusisitiza mahitaji ya makubaliano ya muda mrefu ya kusimamisha vita katika eneo la Idlib, kaskazini magharibi nchini humo.

    prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako