Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ni miongoni mwa viongozi 29 wa nchi zilizokongamana Beijing kupumulia uhai pendekezo la Mkanda Mmoja Njia Moja.
Rais wa China Xi Jinping alipendekeza na kukuza pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja (One Belt One Road) miaka 3 iliyopita, akiutangaza kama kielelezo mpya ya ushirikiano ambayo itachochea maendeleo ya pamoja na mafanikio. Dhahiri, hii imekuwa kipengele muhimu zaidi ya sera za kigeni ya China. Wengi wanautambua kama mchango wa China kwa utaratibu mpya wa dunia.
China imebarikiwa na kanda maalum ambayo imeiweka kwenye kilele cha uchumi duniani. Lakini jimbo la Guangdong kwa wepesi yaonekana kama kichocheo kikuu cha ushawishi wake.
Katika mfululizo wa mipango ya 13 ya China ndani ya miaka mitano (2016-2020), serikali ya China imeweka bayana kwamba inategemea uvumbuzi kuongeza ukuaji wake. Kwa mujibu wa utawala huo wenye makao makuu Beijing, hii itakuza nguvu mpya katika utekelezaji wake wa mikakati ya maendeleo yanayotokana na msukumo wa uvumbuzi.
Sekta ya kilimo inaendelea kupitia mabadiliko mengi. Kuongezeka kwa idadi ya watu duniani inatoa wito wa kuongeza uzalishaji wa chakula. Hata hivyo ahadi hii inaandamwa na vikwazo chungu nzima.
Ni jinsi gani Waafrika ambao husafiri nje ya nchi katika kutafuta malisho mazuri hufanikiwa kuishi kati ya watu wageni kutoka asili mbalimbali pamoja na tamaduni tofauti?
Ubora wa bidhaa zinazotengenezwa kutoka China na kusafirishwa sehemu nyingi duniani, daima zimepokelewa kwa miitikio tofauti. Kwa mara nyingi bidhaa hizo zimedaiwa kuwa na ubora wa hali duni. Afrika kwa upande mwingine imetajwa kuwa mahala ambapo bidhaa hizo zinarundikwa.
Beijing imetangaza kuwa imeboresha ushirikiano wake na Afrika kufikia kiwango cha kina kimkakati. Hii hoja ya karibuni kulingana na maafisa wakuu wa serikali ya China itaharakisha utekelezaji wa malengo muhimu yaliyoandaliwa hasa kuwezesha mataifa ya Africa kuwa bora kiuchumi na kujitegemea.
Mwanzo wa Aprili inadhihirisha mwisho wa majira ya baridi, lakini la muhimu zaidi ni kwamba inatoa fursa kwa msimu mpya wa majira ya machipuko, ambalo ni tukio la kihistoria kwa idadi kubwa ya mataifa duniani.
Kampuni maarufu ya uchapishaji kutoka China sasa inanuia kupanua shughuli zake barani Afrika kuanzia mwaka huu. Kampuni hiyo ya Phoenix Publishing Media Group imetangaza kuwa inatafuta makampuni kutoka bara hilo ili kushirikiana katika sekta ya uchapishaji.
Serikali ya China imefichua kuwa iko tayari kuwekeza zaidi katika bara la Africa. Wizara ya biashara ya nchi hiyo hata hivyo inasema ni wajibu wa nchi za Afrika kutoa taarifa za kutosha kuhusu maeneo ya uwekezaji ambayo usimamizi wa Beijing utaingiza rasilimali zaidi.