• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Migahawa ya kijapani ya mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2008-12-22 15:54:10

    Katika miaka ya karibuni, migahawa ya vyakula vya kijapani inaonekana kwenye sehemu mbalimbali duniani. Mjini Beijing Mikahawa ya kijapani ipo zaidi ya 100, ambayo mingi iko kwenye sehemu za mashariki na kaskazini zenye shughuli nyingi za biashara. Ndani ya majengo makubwa yenye maofisi ya kiwango cha juu yaliyoko karibu na kituo cha biashara ya kimataifa cha Beijing, pia kuna migahawa mingi ya kijapani. Baadhi yake maarufu iliyoko kwenye sehemu hizo ni pamoja na migahawa ya Tokugawake, Sanshiro, Izumo, Mekaku, Wsisshin, Syokusaitei na Edomae Shushi.

    Mgahawa wa Gonibyasyo, ambao ulifunguliwa katika Hoteli ya Beijing mwaka 1985, ni mmoja kati ya migahawa iliyofunguliwa mapema zaidi mjini Beijing. Meneja mkuu wa mgahawa wa Gonibyasyo, Bw. Nagahama Toshikatsu anafahamu sana historia ya maendeleo ya migahawa ya kijapani ya mjini Beijing. Alisema,

    "Tokea miaka ya 80 hadi mwanzoni mwa miaka ya 90, karibu migahawa yote ilifunguliwa katika mahoteli makubwa. Baada ya kipindi cha kati cha miaka ya 90, baadhi yao walifungua migahawa ya kijapani nje ya mahoteli makubwa, vilevile kulikuwa na baadhi ya wachina waliofungua migahawa ya vyakula vya kijapani. Baadhi ya migahawa hiyo ya kiwango cha juu inauza vitoweo vizuri vyenye bei kubwa, vilevile kuna baadhi ya migahawa inauza vitowe vya bei ya chini, kwa mfano, migahawa ya kujihudumia mwenyewe(Do-It-Yourself). Hivi karibuni baadhi ya wanafunzi vijana wa Japan wanaosoma mjini Beijing, walifungua migahawa midogo ya vyakula vya kijapani."


    1 2 3 4 5 6
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako