• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Migahawa ya kijapani ya mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2008-12-22 15:54:10

    Migahawa ya kijapani iliyoko mjini Beijing ni yenye umaalumu tofauti, wateja wanaweza kupata chakula maarufu cha tambi na Sushi asilia za aina mbalimbali. Bw. Takayama Takatusgu, ambaye ni meneja mkuu wa migahawa minne ya kijapani mjini Beijing, alisema, migahawa ya kijapani mjini Beijing inapendwa na watu wengi, watu wanaopenda chakula cha kijapani mjini Beijing wanazidi kuongezeka hivi sasa.

    "Vyakula hasa tunavyouza ni Sushi ya kijapani, na vitoweo zaidi ya aina 100. Hivi sasa Sushi inapendwa sana na watu duniani, nia yetu ni kuwawezesha wateja wapate nafasi ya kula Sushi asilia ya Japani."

    Bw. Takayama Takatusgu alisema, wengi wa wateja wanaokula chakula katika migahawa yetu ni makarani wanaofanya kazi katika kampuni zilizo karibu pamoja na baadhi ya wajapani wanaokaa mjini Beijing, hususan mwisho wa wiki, familia nyingi zinakutana katika migahawa hiyo. Mwanzoni kabisa, watu wengi waliokula katika migahawa ya kijapani ni wajapani, hivi sasa idadi ya wateja wa China inaongezeka kwa mfululizo. Mchina Bi. Wang aliyekuwa akila chakula pamoja na watu wa familia yake katika mgahawa mmoja wa Bw. Takayama Takatusgu, alisema, anapenda sana kula Sushi katika mgahawa huo.Alisema:

    "Chakula cha kijapani cha hapa ni kizuri na cha asilia. Tunakula hapa vilevile tunaweza kufahamu vizuri zaidi utamaduni wa Japani. Hapo awali, sikupenda sana chakula kisichopikwa, kwangu mimi leo ni mara ya kwanza kula Sushi, lakini ninaona ni chakula kizuri, laini sana, tena ni kitamu sana."


    1 2 3 4 5 6
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako