3. Miji yote nchini China hivi sasa ipo kwenye harakati za kukuzwa kiuchumi je, maendeleo ya kiuchumi yakoje katika mji wa Guiyang?
Ikiwa ni mji mkuu wa mkoa wa Guizhou, Guiyang ni sehemu ambayo inajiendeleza kiuchumi, kisiasa, na kiutamaduni, na ili kuboresha uchumi na maisha ya watu, Serikali ya wilaya ya mji huu imetoa kipaumbele kwa elimu ambapo imeanzisha Vyuo vikuu, na hivi sasa ina jumla ya vyuo vikuu vitatu. Lakini mbali na vyuo vikuu mji huu una umeruhusu uwekezaji wa makampuni mbalimbali ya ndani na nje ya China, ambapo wananchi wengi wa Guiyang wamejipatia ajira. Halikadhalika kama nilivyosema awali kuwa mji huu ni wa utalii hivyo kuna sehemu mbali mbali za utalii ambazo zinainua uchumi wa Guiyan kwa ujumla uchumi wa Guiyan kweli umepata maendeleo makubwa.
4. Na vipi kuhusu mtindo wa maisha ya watu wa Guiyang?
Kwa kweli maisha ya watu wa Guiyan hususan wanaoishi nje ya mji huo yamejiegemeza zaidi kwenye mfumo wa maisha ya zamani kwa kufuata mila na desturi za zamani ambazo zinatoa mwamko, haiba na picha nzima ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na makabila madogo madogo yaliyopo Guiyang, ukilinganisha na maisha watu wa miji mingine au hata maisha ya watu wa Guiyan waishio mjini.
Kwenye wilaya ya Guiyan kuna makabila madogomadogo zaidi ya 30 ambayo yana tamaduni tofauti, mingoni mwa makabila hayo ni Miao, Puyi, Dong na Hang. Mfano mavazi wanayovaa makabila haya yanatafautiana au hata mitido ya nywele kwa wanawake pia inatofautiana.
Ahsante sana leo tumepata kujua mji wa Guiyang kwa jumla na katika kipindi kijacho tutajulishwa zaidi kuhusu sehemu mbali mbali za Guiyang alizotembelea Pili Mwinyi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |