• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Migahawa ya kijapani ya mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2008-12-22 15:54:10

    Matembezi ya Bibi Pili Mwini huko Gui Yang

    1 Mbali ya sehemu ulizotalii hapa Beijing lakini pia mwezi wa nane ulitembelea mkoa wa Guizhou na jee unaweza kutuelezea mji wa Guiyan ulivyo.

    Mji wa Guiyan upo katikati ya mkoa wa Guizhou kusini mwa mlima Guishan na ndio mji mkuu wa mkoa huu. Guiyang ina eneo la mita za mraba 8034 na jumla ya watu milioni 36. Mji huu ni mmoja kati ya miji ya china ambayo inavutia sana kwa mandhari nzuri, hali ya hewa nzuri na ina maeneo mengi tu ya vivutio kama vile Hifadhi ya Huaxi, Kumbusho la Zeng Xianyang, mto Qinglong, pamoja na mazingira ya kupendeza vyote hivyo vina historia nzuri na ya kushangaza.

    2. Umeionaje hali ya hewa ya mji wa Guiyan?

    Hali ya hewa ya mji wa Guiyang ni nzuri sana kwani wakati wa kipindi cha majira ya joto hali ya hewa huwa ya kati na kati yaani si joto sana wala baridi sana na kipindi kizuri zaidi cha kutembelea mji huu wa Guiyan ni wakati wa majira ya joto.

    Mji wa Guiyan unastahili hadhi ya kuwa sehemu ya matembezi ya watalii nchini China kwasababu upo kwenye eneo zuri la latitude nyuzi 28 kaskazini ambayo ni karibu na Ikweta, mbali na hilo pia una mwinuko mkubwa upatao mita 1000 kutoka usawa wa bahari.

    Pia Guiyan ina hali ya joto inayokubalika kabisa ambayo ni nyuzi 24 na unyevu asilimia 70 pamoja na upepo wenye mwendo kasi wa

    mita 223 kwa sekunde na vilevile kuna hewa safi kabisa, hivyo vitu vyote hivi vimeufanya mji huu kuwa ni sehemu ya kwanza kwa matembezi ya utalii nchini China.


    1 2 3 4 5 6
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako