Mjini Beijing licha ya kuweko migahawa ya kijapani yenye umaalumu mbalimbali, vilevile kuna baadhi ya matawi ya migahawa ya kijapani inayouza chakula cha haraka. Chakula kinachouzwa katika maduka hayo ni kitamu, na kinatolewa haraka kutokana na kujifunza usimamizi wa maduka ya chakula cha haraka ya nchi za magharibi na Marekani, hivyo yanapendwa sana na vijana wa China na wa nchi za nje.
Mgahawa wa Yuanlu Sushi ulioko kwenye mtaa wa Lishi mjini Beijing ni mgahawa wa kwanza wa Sushi uliofunguliwa mjini Beijing, meneja wake Bi. Ou Fengxia aliwahi kuishi nchini Japani, baada ya kurejea China, alikuwa na wazo la kuwafahamisha wachina vyakula vya kijapani, alisema,
"Chakula kikuu cha hapa bila shaka ni Sushi, halafu ni samaki mbichi aliyekatwa vipande, mkunga aliyeokwa, wali uliotiwa kitoweo juu na tambi. Kuna wageni wengi, ambao wanapenda kula chakula huku wakinywa pombe. Ni vizuri zaidi wakati wa kula Sushi na samaki mbichi aliyekatwa vipande, kutumia pia pombe ya Sake ya japani."
Meneja Bi. Ou Fengxia alisema, mgahawa wake unapendwa sana na vijana wa China, vilevile unapendwa na vijana wa Japan na wa nchi nyingine. Bibi Madrit kutoka Marekani ni mteja aliyefika mara kwa mara katika mgahawa huo, yeye na marafiki zake wanapenda kula chakula cha kijapani katika mgahawa huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |