• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (27 Juni-1 Julai)

  (GMT+08:00) 2016-07-01 17:23:00
  Watano wajitokeza kugombea nafasi ya waziri mkuu wa Uingereza

  Watu watano wamejitokeza kugombea nafasi ya waziri mkuu wa Uingereza baada ya Bw. David Cameron kuamua kujiuzulu.

  Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Bibi Theresa May ameibuka kuwa mgombea mwenye nafasi kubwa zaidi.

  Wagombea wengine ni waziri wa sheria Bw Michael Gove, waziri wa ajira na pensheni Bw Stephen Crabb, waziri wa zamani wa ulinzi Bw Liam Fox na waziri wa nishati Bw Andrea Leadsom.

  Aliyekuwa meya wa London Bw Boris Johnson, ambaye alikuwa anatarajiwa zaidi kushinda nafasi hiyo ametangaza kutogombea.

  Na wakati huo huo Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameitaka Uingereza kufanya maandalizi ya kujitoa haraka katika umoja huo na kuuarifu umoja huo kuhusu kuanza kwa utaratibu husika ili kuepusha kupotea kwa utulivu kwa muda mrefu.

  Mwito huo ulitolewa kwenye mkutano wa viongozi wa nchi 27 za Umoja wa Ulaya bila ushiriki wa waziri mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron uliofanyika jana mjini Brussels, Ubelgiji.

  Akiongea kuwenye mkutano huo Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel amesema Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya ni jambo linalohuzunisha lakini haliwezi kubadilika.

  -

  1 2 3 4 5 6 7 8 9
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako