Rodrigo Duterte aapishwa kuwa rais mpya wa Ufilipino
Rais mpya wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameapishwa rasmi wiki hii na jaji wa mahakama kuu kwenye hafla iliyofanyika katika ikulu ya nchi hiyo.
Baada ya kuapishwa, Duterte ambaye anakuwa rais wa awamu ya 16 alitoa hotuba fupi.
Habari nyingine zinasema, rais Xi Jinping wa China amemtumia salamu za pongezi rais Duterte akisema, anataka kufanya juhudi pamoja na rais huyo ili kuboresha uhusiano kati ya nchi hizi mbili na kutimiza maendeleo endelevu.
Tarehe 9 Mei mwaka huu, uchaguzi mkuu ulifanyika nchini Ufilipino ambapo Bw. Duterte akiwa meya wa mji wa Davao alipata ushindi kwa kupata kura zaidi ya milioni 16.6, na kipindi cha urais wake ni miaka 6.
-
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |