• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (27 Juni-1 Julai)

    (GMT+08:00) 2016-07-01 17:23:00

    Watu 44 wauwawa kwenye shambulizi dhidi ya uwanja wa ndege Uturuki

    Wiki hii watu 44 wamefariki kutokana na shambulizi la mabomu kwenye wa ndege wa Ataturk mjini Istanbul, nchini Uturuki.

    Washambuliaji watatu waliingia kwenye uwanja huo kwa taxi wakafyatua risasi na baadaye kujilipua.

    Zaidi ya wengine 239 wamejeruhiwa, 109 bado wako hospitalini.

    Shughuli za kawaida zilirejelewa kwenye Uwanja huo baada ya masaa machache

    Huku waziri mkuu wa Uturuki Binali Yildirim akitangaza jumatani kuwa siku ya kitaifa ya maombolezi.

    Bado hakuna aliyedai kuhusika na shambulizi hilo, lakini serikali ya Uturuki inalaumu kundi la Islamic State

    Na kwingineko nchini Somalia karibu watu 20 wameuawa baada ya bomu kulipuka na kuharibu kabisa basi walimokuwa wakisafiria katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

    Bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara lililipua gari lililokuwa limewabeba abiria. Wote waliouawa walikuwa raia.

    Mashambulizi hayo yalitokea katika mji wa karibu wa Lafole na inadhaniwa kuwa washambuliaji hao walikuwa wakilenga gari la wanajeshi lililokuwa karibu.

    -

    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako