• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (18 Julai-22 Julai)

    (GMT+08:00) 2016-07-22 18:16:27

    Kundi la waasi la Uganda la LRA laonekana kufufua shughuli zake nchini Afrika ya Kati

    Kundi la waasi la Lord's resistance Army la Uganda (LRA) linaonekana kuimarisha shughuli zake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu kundi hilo limewateka watu 344.

    Ripoti mpya inayofuatilia mwenendo wa kundi hilo imesema kwa ujumla kundi hilo limewateka nyara watu 498, kuwaua 17 katika mashambulizi 122 liliyofanya kati ya mwezi Januari na mwezi Juni mwaka huu. Mashambulizi hayo yote yametokea mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati na Kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Pia kumekuwa na ripoti kwamba baadhi ya mashambulizi yaliyotokea katika maeneo ya Sudan yamefanywa na kundi hilo.

    Mkurugenzi wa Shirika la kimataifa linalohudumia watoto "Invisible Children"Bw Sean Poole amesema kati ya watu waliotekwa nyara kuna watoto 65.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako