• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Agusti 6-Agusti 12)

    (GMT+08:00) 2016-08-12 18:25:13

    Serikali ya Sudan yaupongeza muungano wa vyama vya upinzani nchini humo kwa kusaini makubaliano ya amani

    Serikali ya Sudan imeupongeza muungano wa vyama vya upinzani kwa kusaini makubaliano ya amani na kusema ni uamuzi mwenye busara.

    Makamu wa rais wa Sudan Bakri Hassan Salih amesema hatua hiyo itasaidia kutatuliwa kwa mgogoro unaoikabili nchi hiyo. Amesema baada ya vita kumalizika, nchi hiyo inahitaji maelewano na uvumilivu, na kwamba mazungumzo kati ya pande mbalimbali za nchi hiyo yataendelea kufanyika hadi malengo yake yatimizwe.

    Muungano wa vyama vya upinzani vya Sudan juzi ulisaini makubaliano ya amani yaliyopendekezwa na jopo la utekelezaji la ngazi ya juu la Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako