Ujerumani yachukua hatua kali zaidi za kupambana na ugaidi
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Thomas De Maiziere ametangaza hatua kadhaa za kupambana na ugaidi.
Hatua hizo ni pamoja na kuongeza askari 4600 wa usalama, kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi na ushirikiano ndani ya Umoja wa Ulaya, kudhibiti vibali vya kuishi kwa wageni ambao walikuwa na rekodi ya uhalifu.
Bw. De Maiziere ameeleza kuwa, mpango huo unalenga kuimarisha kikosi cha usalama, kukinga mashambulizi kabla hayajatokea, kusaidia wakimbizi kujiunga na jamii, na kuwaadhibu wahalifu.
Hatua hiyo inakuja baada ya mashambulizi ya mfulululizo yaliyotokea mwezi uliopita nchini humo. Mpaka sasa, polisi wa Ujerumani imetangaza kuwakamata watuhumiwa wanne wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na kundi la IS.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |