• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 22-Oktoba 28)

    (GMT+08:00) 2016-10-28 20:45:30

    Gambia yatangaza kujiondoa ICC

    Gambia imetangaza kwamba itajiondoa kutoka kwa mahakama ya uhalifu ya kimataifa ICC ikiilaumu mahakama hiyo kwa "Mateso na udhalilishaji wa watu wa rangi, hasa Waafrika".

    Waziri wa habari Sheriff Bojang amesema kwenye tangazo la runinga ya serikali kwamba mahakama hiyo (ICC) imekuwa ikiwalenga tu viongozi wa Afrika huku ikikosa kuchukua hatua zozote kwa makosa yanayofanywa na nchi au viongozi wa magharibi.

    Hatua ya Gambia inakuja baada ya nchi nyingine za Afrika Burundi na Afrika Kusini kutangaza kwamba zinajiondoa kwenye ICC.

    Uamuzi wa Banjul, unaelezwa kuwa ni pigo kwa mahakama hiyo pamoja na ofisi ya mwendesha mashtaka Fatou Bensouda, raia wa Gambia ambaye pia aliwahi kuwa waziri wa sheria wa nchi hiyo.

    Hata hivyo Waziri wa mambo ya nje wa Botswana Pelomoni Venson-Moitoi amepinga nchi za Afrika kujitoa ICC.

    Venson-Moitoi anasema kuwa nchi hizo na nchi nyingine za Afrika, badala ya kujitoa kwenye mahakama ya ICC, zinapaswa kuketi na kufanya mabadiliko ambayo wanataka kuyaona ndani ya mahakama hiyo.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako