• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 22-Oktoba 28)

    (GMT+08:00) 2016-10-28 20:45:30

    Afisa wa Ethiopia aasema hali ya dharura inasaidia kutuliza hali nchini humo

    Siku kadhaa zilizopita Ethiopia ilitangaza kipindi cha miezi 6 cha hali ya hatari kutokana na mizozo na mapigano kati ya polisi na jamii ya Oromo nchini humo.

    Wiki hii waziri wa habari wa Ethiopia Bw. Getachew Reda amesema, hali ya dharura inayotekelezwa hivi sasa nchini humo imesaidia kuleta utulivu.

    Pia amesema, bunge la nchi hiyo linatarajiwa kukutana hivi karibuni ili kuupiga kura mswada wa kuifanyia mabadiliko serikali uliowasilishwa na waziri mkuu, lakini hakusema ni lini mabadiliko hayo yatafanyika.

    Tarehe 9 mwezi huu, waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Hailemariam Desalegn alitangaza kuwa nchi hiyo inaingia kwenye hali ya dharura kwa muda wa miezi sita ili kukabiliana na hali ya wasiwasi nchini humo.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako