• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 22-Oktoba 28)

    (GMT+08:00) 2016-10-28 20:45:30

    Umoja wa Mataifa wapitisha uamuzi kwa mara ya 25 kuitaka Marekani iondoe vikwazo dhidi ya Cuba

    Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuitaka Marekani iondoe vikwazo dhidi ya Cuba, ambavyo vimedumu kwa zaidi ya nusu karne.

    Hii ni mara ya 25 kwa Baraza kuu la umoja huo kupitisha azimio kama hilo na Marekani ambayo siku zote iliyapigia kura ya hapana maazimio hayo, kwa mara ya kwanza iliacha kupiga kura. Mbali na Israel ambayo pia haikupiga kura, nchi nyingine 191 wanachama wa Umoja wa mataifa zimekubali azimio hilo.

    Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Liu Jieyi amepongeza kupitishwa kwa azimio hilo na kusema kunaendana na maslahi ya pamoja ya Marekani na Cuba.

    Mwezi wa Julai mwaka jana Marekani na Cuba zilirejesha uhusiano wa kibalozi uliosimamishwa tangu mwaka 1961, lakini vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba bado havijaondolewa.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako