• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 22-Oktoba 28)

    (GMT+08:00) 2016-10-28 20:45:30

    Watu 12 wauawa mjini Mandera kasazini Mashariki mwa Kenya

    Watu 12 wameuawa wiki hii kwenye hoteli ya Bisharo mjini Mandera kasazini Mashariki mwa Kenya, wanasema polisi.

    Mlipuko mitano ilisikika kabla ya ufyatulianaji wa risasi kutokea.

    Wapiganaji wa Al shabaab wanashukukiwa kutekeleza shambulizi hilo la usiku wa kuamkia Jumanne.

    Msimamizi wa nyumba ya malazi iliyoshambuliwa na watu hao wanaodaiwa kuwa wanachama wa kundi la al-Shabaab amekamatwa.

    Bw Abdirahman Bishar Ali, ambaye amekuwa msimamizi wa gesti ya Bisharo amekamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kusaidia katika utekelezaji wa shambulio hilo.

    Stakabadhi ya polisi zinasema Bw Ali hakulala kwenye gesti hiyo kama ilivyo kawaida yake usiku wa shambulio.

    Mkuu wa jimbo la kaskazini mashariki Mohammud Saleh hata hivyo alifutilia mbali uwezekano wa wapiganaji hao wa Al shabaab kutoka Somalia kuwa ndio waliotekeleza shambulio hilo.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako