• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (15 Julai-21 Julai)

  (GMT+08:00) 2017-07-21 19:31:33
  Vijana sita wa Burundi watoweka Marekani

  Vijana sita wa Burundi waliokuwa wakishiriki katika mashindano ya roboti nchini Marekani wameripotiwa kutoweka.

  Polisi wanasema wavulana wanne na wasichana 2 walio kati ya umri wa miaka 16 na 18 walipotea wakati wa mashindano hayo ya kwanza duniani yaliofanyika Washington DC.

  Idara ya polisi mjini humo imesema kuwa mara ya mwisho vijana hao kuonekana ilikuwa siku ya Jumanne wakati wa makamilisho ya michezo hiyo.

  Ripoti zinasema kuwa vijana wawili kati yao tayari wamevuka mpaka na kuingia Canada lakini ripoti hiyo haijathibitishwa na polisi.

  Siku ya Alhamisi, idara ya polisi mjini humo ilibandika picha za sura za vijana hao sita waliopotea katika mtandao wao wa Twitter, wakiwataka raia kuwasiliana nao iwapo watakuwa na habari yoyote kuwahusu.

  Vijana hao wanatambulika kuwa Don Ingabire, Kevin Sambukiza, Nice Munezero, Audry Mwamikazi, Richard Irakoze na Aristide Irambona.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako