• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (15 Julai-21 Julai)

  (GMT+08:00) 2017-07-21 19:31:33

  Mahakama ya ICC kujadili kuachiwa kwa dhamana kwa Laurent Gbagbo

  Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu ICC inatazamia kujadili uwezekano wa kuachiwa huru kwa dhamana kwa aliekuwa rais wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo anaezuiliwa mjini Hague.

  Wanasheria wa kiongozi huyo wa zamani wa Cote d' Ivoire tayari wamewasilisha maombi 11 ya kutaka kuachiwa kwa Laurent Gbagbo kwa kipindi cha miaka kumi na moja na nusu, maombi ambayo yamefutiliwa mbali na mahakama.

  Lakini mnano mwezi Machi, baada ya kukataliwa kwa ombi la kumi na moja, wanasheria wa Gbagbo waliamua kuwasilisha ombi lao mbele ya Mahakama ya Rufaa. Mahakama ya Rufaa inatazamia kutoa uamuzi wake Jumatano hii Julai 19 alaasiri.

  Mpaka sasa, ICC inatoa hoja ya mtuhumiwa huyo kuendelea kusalia kizuizini kwa Laurent Gbagbo, kwa kuhofia kuwa iwapo ataachiwa huru huenda akatoweka, kwa sababu anamtandao mkubwa ambao unaweza kuandaa kutoroka kwake. Laurent Gbagbo anakabiliwa na kifungo cha maisha jela.

  Lakini kwa upande wa utetezi, wanasema hoja hizo hazina msingii. Katika rufaa yao, wanasheria wa Laurent Gbagbo wanaishtumu mahakama kwamba haijaonyesha ushahidi wowote madhubuti wa kuwepo kwa mpango wa kutoroka na kubaini kwamba wateja wao anashikiliwa kizuizini tu kwa kuwa ana umaarufu mkubwa.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako