• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (15 Julai-21 Julai)

  (GMT+08:00) 2017-07-21 19:31:33

  MONUSCO kufunga kambi zake tano Kivu Kaskazini

   

  Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wiki hii tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo (MONUSCO) imefunga kambi tano miongoni mwa kambi zake mkoani Kivu Kaskazini.

  Kivu Kaskazini inakabiliwa na mashambulizi ya makundi mengi yenye silaha.

  Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DR Congo imeondoa idadi ya askari wake waliotumwa katika maeneo ya Masisi na Walikale.

  Lakini pia katika kusini mwa Lubero, pamoja na kufungwa kwa kambi ya Luofu. Hali hii inajitokeza kufuatia kupunguzwa kwa bajeti na ombi la serikali ya DR Congo la kupunguza idadi ya vikosi vya Umoja wa Mataifanchini humo.

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliomba MONUSCO kupunguza askari wake 2,500. Katika mkoa wa Kivu Kaskazini, uamuzi huu umesababisha karibu bataliani yote kuondoka katika maeneo hayo, sawa na askari 750 na makambi yao kufungwa.

  Hakuna tena uwepo wa tume ya kudumu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Walikale, ambapo bado kuna makundi mengi yenye silaha. Kundi jipya lilianzisha hivi karibuni kutokana na mgogoro kati ya wachimba migodi wa jadi na jamii ya Alphamine.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako