• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (15 Julai-21 Julai)

  (GMT+08:00) 2017-07-21 19:31:33

  Rais wa Burundi Piere Nkurunziza afanya ziara nchini Tanzania

  Wiki hii rais wa Burundi Piere Nkurunziza amefanya ziara nchini Tanzania ikiwa ni takriban miaka miwili tangu jaribio la kutaka kupinduliwa kwa serikali yake.

  Rais Nkurunziza amesafiri na mawaziri kadha nchini Tanzania, ambayo imetoa makao kwa zaidi ya wakimbizi 250,000 kutoka Burundi.

  Wakimbizi hao wa Burundi walikita kambi Tanzania kufuatia mzozo uliozuka kutokana na hatua ya Bw Nkurunziza kutaka kuwania urais kwa muhula wa tatu.

  Wakati wa jaribio hilo la mapinduzi lililotendeka mwaka wa 2015, Rais Nkurunziza alikuwa amehudhuria mkutano nchini Tanzania

  Aidha mamia ya wananchi wa Burundi wameuawa tangu ghasia hizo zizuke wengi wakidaiwa kuwa wafuasi wa upinzani.

  Wakati wa ziara hiyo Rais Nkurunziza amewataka warundi waliokimbilia Tanzania kurejea nyumbani kwani sasa kuna amani.

  Rais John Magufuli amempongeza Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi kwa juhudi zake za kusimamia amani nchini mwake.

  Aidha naye ametoa ushauri kwa wakimbizi wa Burundi, kuitikia wito wa Rais wao, wakati marais hao wakihutubia mkutano wa hadhara, uliofanyika kwenye Uwanja wa Posta wilayani Ngara Mkoa wa Kagera.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako