• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( 9 Desemba-15 Desemba)

    (GMT+08:00) 2017-12-15 18:03:15

    Wanajeshi wa Tanzania waliouawa DRC waagwa rasmi

    Hafla ya kuwaaga wanajeshi 14 wa Tanzania waliokuwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa waliouawa nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo imefanyika jiji Dar es Salaam.

    Wanajeshi hao waliuawa baada ya kupigana na waasi kwa muda wa saa 13 kufuatia waasi hao kuishambulia kambi yao.

    Sherehe hizo zimefanyika kwenye makao makuu ya jeshi la ulinzi na usalama Tanzania "gnome" upanga jijini Dar es Salaam

    Mkuu wa ulinzi wa amani wa Umoja wa mataifa Jean Piare Lacroix, alihudhuria sherehe hizo. Familia za wanajeshi hao nazo zilikuwepo na zimeungana na wapendwa wao kuelekea mikoani.

    Shambulio hilo lilitekelezwa Alhamisi jioni kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini.Taarifa ya Umoja wa Mataifa ilisema wanajeshi 5 wa jeshi la DR Congo (FARDC) waliuawa pia kwenye shambulio hilo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako