Maonesho ya kwanza ya ushirikiano wa nishati kati ya China na Afrika yatafuta maendeleo ya pamoja
Maonesho ya kwanza ya ushirikiano wa nishati kati ya China na Afrika yamefunguliwa mjini Nairobi, yakishirikisha viwanda takriban 60 vya China kuonesha teknolojia na vifaa vya kisasa za China katika sekta za ujenzi wa miundo mbinu, mitambo, na upashanaji wa habari, ili kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili na kutafuta maendeleo ya pamoja.
Mkuu wa ujumbe wa China kwenye maonesho hayo Bw. He Cailong ameeleza kuwa, hii ni hatua muhimu katika kutekeleza mipango kumi ya ushirikiano kati ya China na Afrika, na makubaliano yaliyowekwa kwenye Mkutano wa viongozi wa Baraza la ushirikiano wa kimataifa kuhusu "Ukanda mmoja, Njia moja", na kusukuma mbele ushirikiano wa kimataifa katika sekta za nishati na utengenezaji wa vifaa.
Waziri wa ushirikiano wa viwanda na biashara Bw. Adan Mohamed amesema maonesho hayo yameonesha kuwa uhusiano na ushirikiano kati ya China na Afrika unazidi kupata maendeleo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |