• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( 9 Desemba-15 Desemba)

    (GMT+08:00) 2017-12-15 18:03:15

    Askari wasiopungua 18 wa Somalia wauawa katika shambulio

    Zaidi ya askari 18 wa Somalia wameangamia katika shambulio la kujitoa muhanga lilitokea leo Alhamisi katika chuo cha polisi mjini Mogadishu, nchini Somalia, kwa mujibu polisi.

    Katika shambulio hilo askari kadhaa wamejeruhiwa na wengine wako katika hali mbaya.

    Mtu mmoja aliyevalia mkanda wa kulipuka aliingia katika kambi ambako kunapatikana chuo cha polisi, huku akijifananisha na ploisi na kujilipua afisa wa polisi Mohamed Abdulle alisema, huku akibaini kwamba watu wengi wameuawa bila hata hivyo kutaja idadi.

    Kwa mujibu wa mashahidi, polisi wamekua wamekusanyika kwa mazoezi yao ya asubuhi, wakati ambapo mshambuliaji alijilipua.

    Kambi iliyoshambuliwa ni sehemu ya shule kubwa ya polisi nchini Somalia.

    Mpaka sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo.

    Kundi la Al Shabab, lenye mafungamano na al-Qaeda, limekua likitekeza mashambulizi dhidi ya vikosi vya polisi.

    Shambulizi baya zaidi katika historia ya Somalia liligharimu maisha ya watu 512 mnamo Oktoba 14 wakati bomu lililotegwa katika lori bomu lililipuka mjini Mogadishu.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako