• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (23 Desemba-29 Desemba)

  (GMT+08:00) 2017-12-30 16:10:21
  Wizara ya afya nchini Kenya yapiga marufuku uvutaji wa shisha

  Wizara ya afya nchini Kenya ilipiga marufuku uvutaji wa shisha.

  Waziri wa Afya Cleopas Mailu amepiga marufuku uagizaji, utengenezaji utangazaji na uuzaji wa shisha nchini Kenya.

  Kenya sasa ni taifa la tatu kupiga marufuku shisha baada ya Tanzania na Rwanda katika eneo la Afrika mashariki.

  Dkt. Mailu alionya kuwa mtu yeyote atakayepatikana akikiuka sheria za udhibiti wa uvutaji wa shisha atapigwa faini isiopungua shilingi 50,000 za Kenya ama kifungo cha muda usiopungua miezi sita ama zote mbili. Kwa upande wake, mkurugenzi wa huduma za matibabu Jackson Kioko alisema uamuzi huo unatokana na sababu za kiafya na kijamii mbali na ushahidi wa kisayansi kuhusu madhara ya uvutaji wa Shisha.

  Mataifa mengine ambayo yamepiga marufuku uvutaji wa Shisha ni Pakistan, Jordan, Singapore and Saudi Arabia. Shisha hushirikisha bidhaa za tumbaku ambazo hutiwa ladha na huvutwa kwa kutumia mirija kadhaa ilio na maji ambayo moshi wake hupitia kabla ya kumfikia mvutaji.

  Shirika la afya duniani hivi majuzi lilibaini kwamba uvutaji wa Shisha ni hatari kwa afya kwa sababu uvutaji wa sigara 100 ama hata zaidi hufanyika kwa awamu moja wakati mtu anapovuta shisha.

  Nchini Tanzania uvutaji wa Shisha ulipigwa marufuku kutokana na wasiwasi kwamba unahusishwa na dawa za kulevya na pombe.


  1  2  3  4  5  6  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako