• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (23 Desemba-29 Desemba)

    (GMT+08:00) 2017-12-30 16:10:21

    Mahakama ya Cameroon yaamuru kuachiwa huru kwa mwandishi anayedaiwa kumtishia maisha rais

    Jaji mmoja nchini Cameroon ametoa uamuzi wa kuachiliwa kwa muandishi anayeishi Marekani na msomi aliyekamatwa kwa madai ya kumtishia maisha rais Paul Biya.

    Hata hivyo hakuna sababu maalum iliyotolewa kwa uamuzi huo wa kumuachilia huru raia huyo wa Marekani.

    Bw Nganang alikamatwa wiki tatu zilizopita alipokuwa akiondoka katika nchi yake ya kuzaliwa. Ni mkosoaji mkubwa wa Bw Biya kwa miaka 35 ambayo amekuwa uongozoni.

    Serikali inamlaumu kwa kumtishia kumpiga risasi rais Biya kwenye chapisho lake la Facebook. Bw Nganang hakupatikana na hatia wakati alipokuwa mahakamani tarehe 15 Disemba.

    Bw Nganang ni professa wa fasihi kwenye chuo kikuu cha Stony Brook mjini New York.

    Bw Nganang ni muandishi aliyeshinda tuzo ya vitabu vya riwaya ikiwemo ''Temps de Chien", ama "Dog Days" ambayo iliangazia maisha nchini Cameroon chini ya uongozi wa bw Biya.

    Bw Nganang alipokonywa cheti cha usafiri na kukamatwa, alipokuwa akitaka kuabiri ndege kuelekea Zimbabwe.

    Familia yake na marafiki wamesema alikuwa amekamatwa kwa kuandika taarifa kwa gazeti la Ufaransa la Jeune Afrique , akiiikashifu serikali ya Bw Biya jinsi inavyokabiliana na waandamaji na raia wa Cameroon ambao huzungumza Kiingereza.

    Makumi waliuawa mwezi Novemba katika msako uliofanywa kwa waandamanaji.

    Raia wengi ambao hutumia Kiingereza wanawalaumu wengi ambao hutumia lugha ya Kifaransa kwa ubaguzi.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako