• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (23 Desemba-29 Desemba)

    (GMT+08:00) 2017-12-30 16:10:21

    Reli ya Chini kwa Chini mjini Jerusalem kupewa jina Donald Trump

    Waziri wa uchukuzi nchini Israel siku ya alhamisi alitaka kuchimbwa kwa reli ya chini kwa chini kwenye mji wa zamani wa Jerusalem karibu na Ukuta wa Magharibi na kupewa jina la Donald Trump.

    Yisrael Katz alisema anataka kumpa heshima rais huyo wa Marekani kufuatia uamuzi wake wa kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

    Ukuta wa Magharibi ndilo eneo takakatifu zaidi ambapo wayahudi wanaruhusiwa kuomba.

    Reli hiyo mpya ya chini kwa chini na kituo cha treni ni sehemu ya mradi wa reli ya mwendo kasi kutoka Tel Aviv ambayo inatarajiwa kuzinduliwa mwaka ujao.

    Eneo hilo lililo karibu na Ukuta wa Magharibi ambalo hujulikana kwa waislamu kama Haram al-Sharif na kwa wayahudi kama Temple Mount imezua maandamano kutoka kwa wapalestina.

    Hali ya mji wa Jerusalem ndio chanzo cha mzozo kati ya Israel na Palestina.

    Israel inautaja mji wa Jerusalem kuwa mji wake mkuu huku wapalestina wakilitaja eneo la Jerusalem Mashariki lililotwaliwa na Israel wakati wa vita vya mwaka 1967 kama mji mkuu wa taifa lake la baadaye.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako