• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (23 Desemba-29 Desemba)

  (GMT+08:00) 2017-12-30 16:10:21

  Shambulizi Kabul limewaua watu 40

  Ilikuwa ni siku ya huzuni nchini Afghanistan baada ya watu 40 kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa kufuatia milipuko iliyotokea katika kituo cha kitamaduni cha Kishia mjini Kabul. Kundi linalojiita Dola la Kiislamu-IS limedai kuhusika na shambilizi hilo

  Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani amelitaja shambulizi hilo kuwa shambulizi dhidi ya ubinadamu.

  Naibu msemaji wa wizara ya ndani Nasrat Rahimi amesema shambulio hilo lililenga kituo cha kitamaduni cha Tabayan ambacho ni cha Washia, huku akiongeza kuwa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 38 tangu uvamizi wa Kisoviet nchini Afghanistan yalikuwa yakiendelea katika kituo hicho wakati mlipuko ulipotokea.


  1  2  3  4  5  6  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako