• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 14-Aprili 20)

  (GMT+08:00) 2018-04-20 19:33:23
  Mfalme wa Swaziland abadili jina la nchi

  Malme wa Swaziland Mswati III amebadilisha jina rasmi la taifa lake kutoka kuitwa Swaziland na kuibatiza jina jipya la Ufalme wa eSwatini.

  Alitoa tamko hilo wakati wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa ambapo anatimiza miaka hamsini na wakati huo huo taifa hilo likiadhimisha miaka hamsini ya uhuru wake.

  Jina hilo jipya, eSwatini, lina maana ya ardhi ya waswaz na limetumiwa rasmi na Mfalme Mswati wa tatu kwa miaka mingi. eSwati ni jina ambalo mfalme alilitumia alipokuwa akihutubia katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa manmo mwaka 2017 na katika ufunguzi wa bunge la nchini mwake mwaka 2014.

  Mfalme Mswati ni miongoni mwa wafalme wa mwisho wa duniani waliobaki k na ametawala tangu tangu mwaka 1986.

  Wanaharakati wa kutetea usawa wa jinsi wanasema mfumo wa utawala wa nchi hiyo ni wa kushangaza na unawabagua wanawake.

  Mfalme Mswati wa tatu ametoa sababu kuu ya kubadilishwa kwa jina la nchi yake kuwa kila aendapo katika mikutano ya kimataifa, mataifa mengine wamekuwa wakilichanganya taifa lake na nchi ya Switzerland.

  Nao raia wametoa maoni yao juu ya hatua ya mfalme wao na kusema kuwa badala ya kushughulika na jina la nchi yake , badala yake alipaswa kupasua kichwa ni namna gani anaweza kuimarisha uchumi wa nchi hiyo unaodidimia siku hadi siku.

  kwa taarifa yako, Mfalme Mswati anajulikana pia kama Ngwenyama kwa lugha ya taifa hilo jina likiwa na maana ya simba , lakini pia anajulikana ullimwenguni kwa tabia yake ya kuoa wake wengi na kwa kuzingatia mavazi ya jadi pamoja na kuthamini mila na desturi.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako