• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 14-Aprili 20)

  (GMT+08:00) 2018-04-20 19:33:23

  Jeshi la Somalia laua wapiganaji kadhaa wa Al-Shabab kusini mwa nchi hiyo

  Wapiganaji kadhaa wa kundi la Al-shabab wameuawa na wengine kujeruhiwa katika mapigano na jeshi la Somalia SNA likishirikiana na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika katika eneo la Qoqani, jimbo la Lower Jubba kusini mwa Somalia.

  Ofisa mmoja wa jeshi katika eneo hilo Hassan Aden Mohamed amesema, wapiganaji wa Al-Shabab walishambulia kituo cha jeshi kilichoko Qoqani mkoani humo, ambapo jeshi la serikali ya Somalia lilipambana nao. Hakuna vifo na majeruhi kwa jeshi la Somalia na askari wa AMISOM.

  Lakini wapiganaji wa Al-Shabab wametangaza kushinda katika mapambano hayo, na kusema wamedhibiti kambi kadhaa za jeshi la Somalia katika eneo hilo na kuwaua askari kadhaa.

  Wakati huo huo tume ya Umoja wa Afrika ya Kulinda Amani nchini Somalia AMISOM imeitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia Somalia kuijengea uwezo wa kukabiliana na vitisho nchini humo.

  Wakihitimisha mkutano wa nne wa mwaka, Maafisa wakuu wa AMISOM wakiwemo maafisa wa usalama wamefikia makubaliano juu ya hatua za kukabiliana kwa ufanisi na tishio la mabomu ya kienyeji linalozuia mchakato wa kupata utulivu nchini humo.

  Mwakilishi maalum wa mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia Francisco Madeira, amewapongeza washirika mbalimbali kwa kuendelea kuwaunga mkono na kujitolea askari wake kwa AMISOM kukabiliana na tishio la mabomu ya kienyeji (IED) kwa vikosi vya usalama na raia wa Somalia.

  Mapema mwezi huu Kitengo cha Huduma za kutegua Mabomu cha Umoja wa Mataifa kimesema takriban watu 3,000 wameuawa ama kujeruhiwa kutokana na mabomu hayo nchini Somalia.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako