• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 14-Aprili 20)

  (GMT+08:00) 2018-04-20 19:33:23

  Uchaguzi mkuu wa Uturuki kufanyika mwezi Juni

  Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ametangaza kuwa uchaguzi wa rais na wabunge wa nchi hiyo utafanyika Juni 24 mwaka huu, ikiwa ni mwaka mmoja mapema kuliko mpango wa awali wa kufanya uchaguzi mkuu mwezi Novemba mwaka kesho.

  Rais Erdogan amesema Uturuki inaendelea na operesheni za kijeshi nchini Syria, na mabadiliko mapya yametokea kwenye nchi jirani kama Syria na Iraq, hali hizo zote zinahitaji Uturuki ifanye uchaguzi mapema, ili kukabiliana na hali zisizotabirika.

  Mwezi Aprili mwaka jana, Uturuki ilipitisha marekebisho ya katiba yanayompa rais madaraka makubwa zaidi na kufuta wadhifa wa waziri mkuu, ambayo yatatekelezwa rasmi baada ya uchaguzi mkuu kufanyika.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako