• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 14-Aprili 20)

    (GMT+08:00) 2018-04-20 19:33:23

    Sheria ya kufanya ukaguzi bila kibali yapitishwa Burundi

    Bunge nchini Burundi limepitisha muswada wa sheria uliyowasilishwa na Waziri wa Sheria, kuruhusu polisi kufanya ukaguzi katika makazi ya watu bila kibali maalum.

    Hatua hiyo imekosolewa vikali na wapinzani na watetezi wa haki za binaamu nchini humo.

    Mswada huo umepitishwa na sauti 97 na kupingwa na sauti 22 za wabunge wa upande wa upinzani.

    Waziri wa Sheria Aimé Laurentine Kanyana aliutetea muswada huo kwa kile alichokitaja kuwa Burundi unakabiliwa na visa vya mauaji ya kikatili,ugaidi, baishara ya binadamu na kumiliki silaha kinyume cha sheria, utumiaji wa dawa za kulevya na hata ubakaji.

    Hata hivyo,msako wa mchana hautohitaji kibali maalum,vikosi vya usalama vitaweza kuendesha msako wakati wowote.

    Lakini, msako wa usiku utahitaji kibali maalum cha Kamishna wa polisi au idara nyingine husika.

    Vyama vya upinzani nchini humo, vimehofia utaratibu huo, ambapo mkuu wa chama cha upinzani ,UPRONA , Abel Gashatsi amesema Burundi imetoka katika vita.

    Kwa upande wa chama kikongwe cha upinzani, FRODEBU wanasema muswada huo unakiuka katiba na kupendekeza baraza la Seneti kuurejesha na kuipinga.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako