• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 14-Aprili 20)

    (GMT+08:00) 2018-04-20 19:33:23

    Askari auawa,20 wajeruhiwa baada ya shambulizi Timbuktu nchini Mali

    Shambulizi la roketi na bomu lililotegwa garini limeua Askari mmoja wa kulinda amani nchini Mali na kujeruhi wengine kadhaa wa kikosi cha Ufaransa Mjini Timbuktu nchini Mali maafisa wameeleza.

    Kulingana taarifa ya wizara ya ulinzi nchini Mali iliyochapishwa katika ukurasa wa FB shambulizi la kigaidi lililenga kambi ya kijeshi ya ufaransa na jeshi la UN nje ya mji wa kaskazini jumamosi mchana.

    Washambuliaji wawili waliovalia kama askari wa umoja wa mataifa wakiwa na pikipiki walishambulia kwa maroketi kambi hizo mbili.

    Wizara ya ulinzi nchini Mali imesema askari mmoja ndie alipoteza maisha na majeruhi kutoka jeshi la Ufaransa watano wakiwa katika hali mbaya.

    Awiki hii China itatuma walinzi 395 wa amani nchini Mali mwezi Mei kuhudumia Tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

    Imethibitishwa kuwa batalioni hii yenye askari 170 wa ulinzi, askari 155 wa uhandisi na wengine 70 wa matibabu, itakuwa ni kikosi cha sita cha walinzi wa amani wa China kupelekwa nchini Mali, na kutekeleza majukumu ya kukarabati miundombinu, kulinda makao makuu kwenye maeneo ya vita, na kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa na majeruhi.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako