• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 14-Aprili 20)

    (GMT+08:00) 2018-04-20 19:33:23

    Maelfu ya wauguzi wanaogoma wafukuzwa kazi Zimbabwe

    Serikali ya Zimbabwe imetangaza kwamba imewafukuza kazi maelfu ya wauguzi wanaoendelea na mgomo wakidai kulipwa mshahara mzuri.

    Makamu wa Rais Constantino Chiwenga amewashtumu wauguzi hao kwamba walishawishiwa kisiasa

    Wagonjwa hawakuweza kuelekea hospitali kuu wiki hii baada ya mgomo wa wauguzi kuanza. Mgomo huo ulianza wiki kadhaa tu baada ya mgomo wa madaktari.

    Makamu rais wa Zimbabwe aliongeza kuwa wauguzi wasio na ajira na wastaafu wanatajiria kuchukua nafasi ya wale waliofukuzwa kazi.Jenerali Chiwenga aliongoza operesheni ya kung'olewa kwa rais Robert Mugabe mnamo mwezi Novembea 2017 wakati jeshi lilipochukua kwa muda mfupi udhibiti wa nchi kabla kuteuliwa kwa rais Emmerson Mnangagwa.

    Jenerali Chiwenga amesema anasikitishwa na mgomo wa wauguzi wakati ambapo serikali ilitoa dola milioni 17 ili kuboresha mishahara yao. Chiwenga ameongeza kwamba sasa pesa hizi zitatumika kwa kulipa mishahara ya wauguzi wapya.

    Chama cha Wauguzi nchini Zimbabwe kimesema kuwa "kimepokea" taarifa ya Chiwenga lakini kitaendelea na mgomo.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako