• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 5-Mei 11)

  (GMT+08:00) 2018-05-11 18:46:31
  Watu 42 wafariki baada ya kuvunja Kenya

  Watu 42 wamefariki na maelfu wengine wameachwa bila ya makaazi wakati bwawa moja kaunti ya Nakuru nchini Kenya lilipovunja kuta zake Jumatano usiku.

  Wakaazi wanasema watu wengine zaidi hawajulikani waliko.

  Bwawa la Patel mjini Nakuru katika mkoa wa bonde la ufa lilivunja kuta zake jana usiku na kusomba mamia ya nyumba za wakaazi waliokuwa karibu na eneo hilo.

  Waziri wa mambo ya ndani Kenya Fred Matiangi amewasili katika eneo hilo.

  Walioshuhudia wanasema walisikia mshindo mkubwa kabla ya mawimbi makubwa kuyasomba makaazi na mashamba ya watu yenye umbali wa takriban kilomita mbili, eneo ambalo watu wengi wanaishi na kufanya kazi.

  Kuna hofu kwamba huenda idadi ya watu waliofariki ikaongezeka wakati jitihada zikiendelea za kuwatafuta na kuwaokoa manusura.

  Huu ni mkasa wa kwanza wenye ukubwa wa aina hii kuwahi kushuhudiwa Kenya.

  Zaidi ya watu 2000 wameachwa bila ya makaazi.

  Bwawa hilo la Patel ni mojawapo ya mabwawa matatu yanayomilikiwa na mkulima mmoja mkubwa katika eneo hilo.

  Inaarifiwa kwamba kuta zake zilibomoka kutokana na maji mengi yaliokusanyika kufutia mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini.

  Viongozi wa eneo hilo sasa wanataka kujuwa iwapo mkulima huyo ana kibali kilichomruhusu kujenga mabwawa hayo, huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hali ya mabwawa mawili yaliosalia ambayo pia yanatajwa kuwa yamejaa.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako