• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 5-Mei 11)

  (GMT+08:00) 2018-05-11 18:46:31

  Burundi kusimamisha matangazo ya BBC na VOA

  Baraza la Vyombo vya Habari la Taifa la Burundi litasimamisha matangazo ya Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC na Sauti ya Marekani VOA katika maeneo yote nchini humo kwa miezi sita, uamuzi ambao utaanza kutekelezwa tarehe 7, Mei.

  Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Ramadhan Karenga, BBC imekiuka kanuni za "uwiano wa taarifa" na "thibitisho kali" la vyanzo vya habari kwa mujibu wa sheria ya vyombo vya habari ya Burundi.

  Amesema VOA imechukuliwa hatua hiyo kutokana na kuendelea kutoa vipindi kwa kituo cha radio kilichosimamishwa tangu mwaka 2015. Pia VOA imemwajiri mwanahabari mmoja wa Burundi anayekabiliwa na hati ya kimataifa ya kukamatwa.

  Radio ya kimataifa ya Ufaransa RFI na vituo viwili vya radio vimepata onyo kutokana na kukiuka sheria ya vyombo vya habari vya Burundi.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako