• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 5-Mei 11)

  (GMT+08:00) 2018-05-11 18:46:31

  Korea Kaskazini yawaachia huru raia wa Marekani

  Korea Kaskazini imewaachia huru raia watatu wa marekani kutoka gerezani, ukurasa wa tweeter wa Rais wa Marekani Donald Trump umeeleza.

  Hatua hiyo inaonekana kama dalili njema kuelekea mkutano wa kihistoria kati ya Rais Trump na mwenzie wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

  Kim Hak-song, Tony Kim and Kim Dong-chul walikuwa kifungoni baada ya kukutwa na hatia ya kufanya vitendo viovu dhidi ya serikali.

  Rais Trump ametangaza kuachiwa kwao siku ya Jumatano.

  Ikulu ya Korea Kusini imeunga mkono kuachiwa huru kwa raia wa Marekani, ikisema ni ishara njema wakati wakielekea kwenye mazungumzo.

  Msemaji wa Ikulu Yoon Young-chan pia ametoa wito wa kuachiwa kwa raia wao sita walioko kifungoni.

  Wakati huo huo Rais ya wa Marekani Donald Trump ametangaza Jumanne kwamba nchi hiyo inajiondoa kwani Makubaliano hayo hayawezi kuzuia Iran kutekeleza shambulizi la nyuklia.

  Aidha Trump amesema Marekani inaongeza vikwazo dhidi ya Iran.

  Hata hivyo rais wa IranHassan Rouhani amekosoa hatua ya Marekani kujitoa na kudai kuwa haiheshimu makubaliano yake.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako