• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 5-Mei 11)

  (GMT+08:00) 2018-05-11 18:46:31

  Tanzania yafungua ubalozi Israel

  Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt. Augustine Mahiga amezindua rasmi ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Israel na kuitaka Israel nayo iharakishe kufungua ofisi ya ubalozi nchini Tanzania.

  Afisi hizo za kibalozi zinapatikana katika mji wa Tel Aviv.

  Rais John Magufuli mwezi Machi mwaka huu alikuwa amemualika Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutembelea Tanzania na pia kuanzisha ofisi ya ubalozi nchini Tanzania badala ya kutumia ofisi za ubalozi zilizopo Nairobi nchini Kenya.

  Waziri Mahiga, akizindua ubalozi huo Jumanne, alisema Watanzania hawataisahau Israel kwa kuwa ndiyo nchi iliyoisaidia Tanzania kuanzisha Jeshi la Kujenga Taifa ambalo mafanikio na mchango wa jeshi hilo unajulikana na kila Mtanzania.

  Dkt Mahiga alisema Israel ni nchi ya kupigiwa mfano kwa sababu licha ya changamoto za kimahusiano na baadhi ya jirani zake bado nchi hiyo imepiiga hatua kubwa za kimaendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo cha umwagiliaji.

  Aidha, imepiga hatua katika sekta ya viwanda, matibabu, teknolojia ya habari na mawasiliano, ulinzi na usalama, uhifadhi wa maji na masuala ya nishati ikiwemo nishati ya kutumia joto ardhi.

  Ufunguzi wa ubalozi huo ni muendelezo wa juhudi za kuimarisha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili ambazo zilitiwa nguvu na ziara ya mawaziri wawili wa Israel nchini Tanzania mwezi Machi.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako