• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 5-Mei 11)

  (GMT+08:00) 2018-05-11 18:46:31

  Viongozi wa China, Japan na Korea Kusini watoa taarifa ya pamoja

  Mawaziri wakuu wa China na Japan Bw. Li Keqiang na Bw. Shinzo Abe, pamoja na rais Moon Jae-in wa Korea Kusini jana walihudhuria mkutano wa saba kati ya viongozi wa pande hizo tatu mjini Tokyo, Japan, na kutoa taarifa ya pamoja.

  Taarifa inasema viongozi wa nchi hizo tatu wanapongeza juhudi za jumuiya ya kimataifa katika kuboresha hali ya Peninsula ya Korea.

  Pia wamesifu na kukaribisha azimio la Panmunjom lililosainiwa kwenye mazungumzo yaliyofanyika tarehe 27 Aprili kati ya viongozi wa Korea Kusini na Korea Kaskazini Bw. Moon Jae-in na Bw. Kim Jong-un, ambalo limeweka bayana lengo la pamoja la kutimiza Peninsula ya Korea kuwa sehemu isiyo na silaha za nyuklia na kuanzisha utaratibu wa amani ya kudumu.

  Taarifa pia imesema viongozi hao wanatumai pande zote zinazohusika zitaendelea na juhudi za kulinda amani na utulivu wa kikanda kwa msingi wa mazungumzo.

  Awali Mei 7 rais wa China Xi Jinping alikutana na kiongozi wa Korea Kaskazini katika mji wa Dalian mkoa wa Liaoning.

  Wawili hao walijadili kwa kina maswala ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako