• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 19-Mei 25)

    (GMT+08:00) 2018-05-25 20:00:01

    Kenya yavumbua dawa ya Malaria kwa wanawake waja wazito

    Ilikuwa ni wiki nzuri nchini Kenya baada ya Wanasayansi katika taasisi ya utafiti wa afya nchini Kenya KEMRI kufanyia utafiti dawa mpya ya kuzuia Malaria kwa wanawake waja wazito.

    Dawa hiyo, dihydroartemisinin-piperaquine (DP), ilifanyiwa majaribio katika maeneo tofauti nchini Kenya ikiwemo, Ahero magharibi mwa nchi, na imegunduliwa kuwa salama kwa matumizi ya kuzuia Malaria kwa wanawake walio na miezi kati ya 4 hadi 9 ya uja uzito.

    Ugonjwa wa Malaria una hatari kubwa zaidi kwa wanawake waja wazito. Miezi mitatu ya kwanza ya uja uzito ndio wakati ambapo watoto wachanga wanakabiliwa na hatari kubwa za athari zinazotokana na dawa za Malaria.Kwa mujibu wa shirika la Afya duniani, ugonjwa wa Malaria unaendelea kusababisha vifo vya watu kadhaa.

    Mnamo 2016, watu 445 000 walifariki kutokana na Malaria duniani ikilinganishwa na 446 000 mnamo 2015. Inakadiriwa kwamba ugonjwa huo husababisha vifo vya watoto wawili kila dakika mbili.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako