• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 19-Mei 25)

    (GMT+08:00) 2018-05-25 20:00:01

    Mwanaume mmoja alishtaki kanisa nchini Uganda kupinga kanuni za utaratibu wa kufunga ndoa

    Ilikuwa ni hatua ambayo iliwashangaza wengi pale Mwanaume mmoja alipolishtaki kanisa moja nchini Uganda kupinga kanuni za utaratibu wa kufunga ndoa akieleza kuwa zinakwenda kinyume na katiba.

    Michael Aboneka alipeleka kesi hiyo katika mahakama ya katiba mjini Kampala kulishtaki kanisa la Watoto Church wakati waumini wengine wa kanisa hilo wakiunga mkono taratibu za kanisa lao.Michael Aboneka amesema kuwa Watoto Church, linawanyima vijana wengi haki yao ya kikatiba ya kufunga ndoa na wapenzi wao baada ya kutimiza umri wa miaka 18 kama katiba ya Uganda inavyosema.

    Ameeleza kuwa baada ya kuzisoma kanuni hizo za kufunga ndoa, ameona kuwa zinakwenda kinyume na katiba. Aboneka amesema kuwa siyo kwamba ana chuki na kanisa la watoto, ila ni kusaidia vijana wengi ambao wameshindwa kufunga ndoa zao ili mahakama ya katibu itowe ufumbuzi wa swala hilo.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako