• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 19-Mei 25)

  (GMT+08:00) 2018-05-25 20:00:01

  Korea Kaskazini yasema iko tayari kukutana na Trump

  Tukiiingia kwenda uwanja wa kimataifa tunaangazia vuta nikuvute kati ya Korea kaskazini na Marekani ambapo wiki hii Korea Kaskazini ilielezea kusikitishwa kwake na hatua ya rais Donald Trump kujitoa katika mazungumzo yaliyopangwa kufanyika juni 12 huko Singapore.

  Kwa mujibu wa mashirika ya habari nchini humo, uamuzi huo umekuwa kinyume na matarajio ya dunia.

  Inadaiwa kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un alikuwa amefanya jitihada zote katika maandalizi ya mkutano huo na kwamba nchi hiyo ilikuwa tayari kuhakikisha tofauti zilizopo kati ya taifa lake na Marekani zinasuluhishwa kwa namna yoyote na popote, lakini Trump mwenyewe amesema uwezekano wa kufanyika mazungumzo hayo bado upo.

  Taarifa hizo pia zimeleta mshtuko kwa jumuiya ya kimataifa, ambapo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres, ameelezea kuguswa kwake na hatua hiyo ya Marekani huku naye rais wa Korea Kusini Moon Jae-In akitoa wito kuwepo kwa mkutano wa dharura wa viongozi wa juu wa usalama kuhusiana na suala hilo. Mkutano huo ungejadili namna ya uondoaji wa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea kufuatia mkutano wa Korea zote mbili uliofanyika mwezi April mwaka huu.

  Hata hivyo yapo baadhi ya mambo yanayotajwa kama dosari zilizojitokeza kuelekea kwenye mazungumzo hayo.


  1  2  3  4  5  6  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako